MSHAMBULIAJI Diego Forlan usiku wa
kuamkia leo amesherehekea mechi yake ya 100 Uruguay kwa kufunga bao la
ushindi timu yake ikishinda 2-1 dhidi ya Nigeria kwenye Kombe la Mabara
mjini Salvador.
Forlan alifunga mwanzoni mwa kipindi cha
pili baada ya John Obi Mikel kuisawazishia Nigeria dakika ya 37
kufuatia Uruguay kufunga bao la kuongoza dakika ya 19 kupitia kwa Diego
Lugano.

Forlan akishangilia na mwenzake

Diego Lugano akipongezwa na wenzake

Matokeo hayo yanafanya timu mbili katika
Kundi hilo, B zilingane kwa pointi, tatu kila moja baada ya kucheza
mechi mbili, lakini ikiwa imebakiza mechi na Tahiti, Uruguay iko katika
nafasi kubwa ya kusonga mbele pamoja na Hispania, yenye pointi sita na
itacheza na Nigeria katika mechi ya mwisho ya kundi hilo.
KUNDI B KOMBE LA MABARA
Timu | Mechi | Kushinda | Sare | Kufungwa | Mabao ya Kufungwa | Mabao ya kufungwa | Pointi |
---|---|---|---|---|---|---|---|
Hispania | 2 | 2 | 0 | 0 | 12 | 1 | 6 |
Nigeria | 2 | 1 | 0 | 1 | 7 | 3 | 3 |
Uruguay | 2 | 1 | 0 | 1 | 3 | 3 | 3 |
Tahiti | 2 | 0 | 0 | 2 | 1 | 16 | 0 |

John Obi Mikel (kulia) akishangilia baada ya kufunga

Martin Caceres wa Uruguay akimdhibiti Ahmed Musa
0 comments:
Post a Comment