Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 February 2017
Wednesday, February 01, 2017

HENRY AMPIGIA DEBE GRIEZMAN EPL

Na FLORENCE GR

Kwa kile kinachoonekana kama kumpigia debe mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Thiery Henry amsema kuwa angependa kumuona mfaransa mwenzake Antoine Griezman anaekipiga katika klabu ya Athletico Madrid ya Hispania akicheza katika ligi kuu ya nchini Uingereza.

Akijibu katika kituo cha Sky sport mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal na Ufaransa amesema kuwa 'Nafikiri huyo ni mtu anaetakiwa kuja kucheza ligi kuu'.

'Kama akienda OT kitakuwa kitu kikubwa  kwao lakini  ni mchezaji unae muhitaji kwenye ligi, mashabiki na kila kitu anataka kumuona akicheza hapa'.

Henry ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa Arsenal amesema kuwa amekuwa akimfuatilia Griezman kwa muda mrefu  tangu alipokuwa mdogo akiichezea timu ya Sociedad baada ya kukataliwa kukipiga katika timu ya vijana ya  Lyon ya nchini Ufaransa huku akisema si lazima mchezaji huyo achezee man united tu.

Griezman ni mmoja wa wachezaji wenye vipaji katika ulimwengu wa soka huku mwaka 2016 ukiwa wa mafanikio kwake huku akifanikiwa kuingia kwenye tuzo kubwa kabisa duniani na kufanikiwa kushika namba tatu katika tuzo hizo ambazo ni Ballon d'Or na ile ya mchezaji bora wa FIFA.

 Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alikuwa akihusishwa kujiunga na Manchester united kwenye dirisha la usajili lililofungwa jana anamkataba na Athletico hadi mwaka 2021 huku akisema kuwa anafuraha kucheza chini ya  Diego Simeone.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!