Searching...
Image and video hosting by TinyPic
10 September 2014
Wednesday, September 10, 2014

Uholanzi yaangukia pua.


Na Chicoti (Cico cicod)
 0755 700 076


Kocha mpya wa Uholanzi Guus Hiddink aanza vibaya mechi za kufuzu mashindano ya bara la ulaya kwa mwaka 2016 maarufu kama EURO baada ya kuchapwa kwa magoli 2-1 dhidi ya Czech Republic katika mechi iliyopigwa jijini Prague. 

Czech waliandika goli la kwanza dakika ya 32 kupitia kwa Borek Dockal aliyepokea pasi kutoka kwa David Lafata, goli lililoamsha kelele toka kwa mashabiki waliojazana kwenye uwanja wa Generali Arena.

Uholanzi waliomkosa mshambuliaji wao hatari Arjen Robben waliweza kusawazisha dakika ya 55 kupitiwa kwa stefan de Vrij aliyeunganisha krosi iliyochongwa na Daley Blind. Mpira ukikaribia kuisha Czech walipata goli la pili na la ushindi kwenye dakika ya 90.

Bao hilo lilitokea baada ya Kosa lililofanywa na beki wa kulia wa Uholanzi anayekipiga kwenye timu ya Newcastle Daryl Janmaat kushindwa kuupiga mpira vizuri kwa kichwa kuurudisha kwa kipa Jasper Cillessen na mpira kugonga nguzo ya goli kabla kumkuta Vaclav Pilar aliyeipatia Czech Republic goli la ushindi. 

Guus Hiddink anayeifundisha Uholanzi kwa mara ya pili baada ya mechi alipohojiwa na waandishi wa habari huku akionekana kutofurahishwa na matokeo hayo alisema “Nina hasira, katika sekunde za mwisho wa mechi, hutakiwi kupoteza” aliendelea kusema “tungeweza kuondoka hapa na sare ya 1-1 ila tumeshindwa kwa uzembe wetu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!