Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 April 2014
Monday, April 21, 2014

BAYERN WANALILIA BAO LA UGENINI MBELE YA REAL MADRID




 Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Mwenyekiti wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge anasema mabingwa hao wa Ulaya sharti waonyeshe sifa za lakabu yao ya “Wanyama weusi” watakapokutana na Real Madrid Jumatano kwenye mechi ya kwanza ya nusufainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. 

Mashabiki wa Real wamewapa Bayern jina la utani la "la bestia negra" (Wanyama weusi) au "Bete Noire" baada ya mfululizo wa vichapo kutoka kwa miamba hao wa Ujerumani, cha juzi zaidi kikiwa nusufainali ya Ligi ya Mabingwa 2012, ambayo iliamuliwa kwa mikwaju ya penalti Madrid. 

Bayern wameshusha uchezaji wao na wameshinda mechi tatu kati ya saba walizocheza majuzi tangu washinde taji la Bundesliga mwezi jana wakiwa wamesalia na mechi saba za kucheza, ambayo ni rekodi. Rummenigge anataka kuona timu hiyo ikionyesha ukali wake zaidi dhidi ya Madrid. 

"Tunajilikana kama 'la bestia negra' huko na tunahitaji kuwaonyesha kwamba 'la bestia negra' wamerudi," akasema Rummenigge baada ya ushindi wa Bayern usio wa kuridhisha wa 2-0 katika Bundesliga dhidi ya timu inayoshika mkia ya Eintracht Braunschweig Jumamosi. 

Rummenigge amewataka wachezaji hao wawe na ujasiri – na wapate angalau bao moja la ugenini mechi hiyo ya kwanza Madrid.
“Tunahitaji kufunga angalau goli moja. Hayo ndiyo tulijifunza kutoka kwa mechi za Dortmund na Real Madrid,” akaongeza baada ya Borussia Dortmund kubanduliwa kutoka Ligi ya Mabingwa, licha ya ushindi wa 2-0 robofainali nyumbani, baada yao kushindwa 3-0 wakiwa Madrid. 

Bayern waliimarishwa Jumapili baada ya kipa wa Ujerumani Manuel Neuer kurudi mazoezini baada ya kukosa mechi mbili zilizotangulia kutokana na jeraha la misuli ya chini ya mguu na pia beki wa kushoto David Alaba aliyerudi baada ya kukosa mechi ya Braunschweig kutokana na mafua. 

Bado haijabainika kama nyota wa Real Cristiano Ronaldo atakuwa sawa kucheza mechi hiyo ya Bernabeu, lakini Rummenigge amesema anapenda sana nyota huyo wa Ureno aongoze mashambulizi ya Real wakiwa Madrid. 

"Mechi hiyo ya nusufainali ni kubwa na itatazamwa na watu kila pembe ya dunia. Kwa hivyo tunataka kuona wachezaji wote wazuri,” akaongeza Rummenigge

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!