Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 August 2013
Wednesday, August 07, 2013

MANJI AITISHA MKUTANO WA DHARURA

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameitisha mkutano wa dharura wa wanachama tarehe 18 Agosti, 2013 utakaofanyika uwanja wa Sabasaba kwenye ukumbi wa PTA saa 3.30 asubuhi kujadili sakata linaloendelea kuhusu michezo ya Ligi Kuu kurushwa katika kituo cha Azam TV. 
 
Yanga ilitoa msimamo wake wa kupinga michezo inayoihusu kurushwa na kituo hicho huku TFF ikisisitiza maamuzi yaliyofikiwa na kamati ya ligi na wawakilishi wa klabu nyingine wakiiponda Yanga. 
 
Sehemu ya barua iliyotumwa kwa vyombo vya habari inasema "Kwa kuwa YANGA ni Klabu ya Wanachama yenye kupata nguvu kutokana na misingi yake ya kidemokrasia iliyojijengea na uamuzi wake wa mwisho unatokana na Wanachama wake mwenyewe, umeamua kuliweka suala hili zima kwa Wanachama wa Yanga ili waamue ni njia gani ya kufuata kwa maslahi ya Klabu yetu".

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!