NIONAVYO MIMI KWA PODOLSKI SIMLAUMU WENGER
Kuna uwezekana mkubwa sana kocha wa arsenal,arsene wenger aligundua
mapema kwamba RVP ataondoka msimu uliopita na ndio maana usajili wa
mjerumani Lukas Podolski aliyezaliwa mwaka 1985 ulifanyika mapema sana.
Bundasliga ni ligi bora ambayo tunaamini inatumia nguvu sana ingawa
siku za hivi karibuni inaonekana kubadilika na kucheza mpira wa pasi na
nafasi kama Hispania na Brazil ile ya zamani.Ukiniambia Podolski
anahitaji kuzoea EPL,mimi sikubali.
wenger alipomsajili LUKAS PODOLSKI wengi tuliamini ni usajili mzuri kwa
sababu POLD ananguvu,mbio,uzoefu na yale mashuti yake ya MBAGALA hadi
SINZA tukajua wenger amepatia.
PODOLSKI kamuangusha wenger,kwa
uwezo wake na uzoefu nadhani angeweza kuziba pengo la RVP.Amemfanya kuwa
mchezaji anayelipwa zaidi pale EMIRATES lakini amekuwa ni mchezaji
ambaye hata kumaliza dk 90 ni mbinde.
No comments:
Post a Comment