Hatimaye Coastal Union yanasa saini ya mchezaji kutoka Kenya.
Mwakilishi wa Coastal Union nchini Kenya Hussein Tawakkal akikamilisha
zoezi la usajili la mchezaji kutoka Bandari ya Mombasa na Harambee Stars
ya Kenya CRISTIN ODULA WADENYE kwa mkataba wa kuwachezea Wagosi kwa
miaka miwili jana jijini Mombasa.......huyu ni mchezaji ambae kocha wetu
Hemed Morocco akililia kwa udi na uvumba apatikane tena kwa gharama
yoyote ili aje kutengeneza 'combination' hatari katikati wakisaidiana
na Jerry Santo na Haruna Moshi 'Boban'.............wapinzani kaeni mkao
wa kuliwa.........!!!!!
Mkurugenzi wa ufundi wa Wagosi wa Kaya Nassor Ahmed 'Binslum' mwenye
kofia akiwa na kiungo mshambuliaji kutoka Bandari ya Mombasa aliyesaini
kuungana na kikosi cha Coastal Union CRISTIN ODULA (katikati), kulia ni
mwakilishi wa Coastal Union jijini Mombasa Kenya ndugu Hussein Tawakkal.
Coastal Union sasa imebakisha mchezaji mmoja tu katika safu ya
ushambuliaji baada ya kufanikiwa kunasa saini za wachezaji kumi watatu
wakitoka timu ndogo. Msimu ujaoo mmhhh we acha tu.
No comments:
Post a Comment