AMR KIEMBA ASAINI MKATABA MIAKA MIWILI MBELE KUUZWA MOROCCO
Klabu ya Simba ya Dar es Salaam imetangaza kufikia makubaliano ya
kuongeza mkataba na kiungo anayesadikiwa kua bora kabisa kwa sasa
Tanzania Amri Kiemba.
Mchezaji huyo ambaye alicheza vizuri sana
dhidi ya Morocco huku akitupatia bao pekee alilofunga kwa ustadi mkubwa
hata kufanya klabu za Morocco kuanza kutaka mazungumzo ya kumsajili
kiungo huyo kitu ambacho Simba wameshaanza kukichangamkia.
Mara baada ya kurejea kutoka katika mchezo dhidi ya Morocco jana Simba
ilikuwa kwenye jitihada nzito kuhakikisha inamzuia Kiemba kusaini Yanga
kwa kumpa ofa nono ya mkataba mpya, Kiemba alikuwa akihitaji kiasi cha
millioni 38 ili asaini msimbazi lakini baada ya mazungumzo marefu Kiemba
amekubali kusaini kwa kiasi cha millioni 35 kwa miaka miwili.
Pia Kiemba atakuwa analipwa mshahara wa millioni 2 kwa mwezi. Alisaini
mkataba huo mbele ya kaimu makamu mwenyekiti Mzee Kinesi.
Mkurugenzi wa masuala ya usajili Simba akiongea kutokea Arabuni
alipokwenda kufuatilia pesa za ada ya uhamisho wa aliyekua mchezaji wa
klabu hiyo Emmanuel Okwi alithibitisha kwenye redio fulani hapa Dar es
Salaam kwamba Simba nia yao ni kumuuza na hata mkataba walioingia nae ni
kwa kua wana uhakika wa kumuuza huko Arabuni.
Pia alidai
ameshapokea mualiko wa kwenda kulizungumzia suala la uhamisho wa Kiemba
huko Morocco na baada ya kumaliza masuala ya pesa za usajili za Okwi
atarejea Morocco kwa suala la Kiemba.
Unadhani ni vizuri kumuuza ili kupata fedha zitakazojenga timu zaidi au kumtumia kwa msimu huu ili kurudisha heshima yao?
No comments:
Post a Comment