Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 February 2015
Tuesday, February 03, 2015

Fletcher, Zaha waondoka United.

Na Chikoti Cico

 
Dirisha dogo la usajili lililofikia tamati usiku wa jana limeshuhudia klabu ya Manchester United ikiwauza wachezaji wake wawili kiungo mkongwe Darren Fletcher na winga Wilifried Zaha .

Fletcher ambaye amesajiliwa na klabu ya West Bromwich Albion kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu alikamilisha usajili huo baada ya muda wa usajili kuongezwa. Mkataba wa kiungo ni miaka miwili na nusu kwa matarajio ya kuongezewa miezi 12 zaidi.

Taarifa kutoka nchini Uingereza zinasema Fletcher alikuwa asajiliwe na klabu ya West Ham lakini dili hilo lilikufa baada ya kocha wa West Ham Sam Allardyce kutaka kumsajili kiungo huyo kwa mkopo badala ya mkataba wa moja kwa moja jambo ambalo kocha wa Man United Louis van Gaal hakulitaka na ndipo West Brom wakafanikiwa kumsajili.

Akiongea na mtandao wa West Brom baada ya kukamilisha usajili huo Fletcher alisema “najiskia vizuri, hii ni changamoto nzuri kwangu kwenye soka langu".

Aliendelea kusema kuwa "Nimetumia soka langu pale Manchester United na hilo ndilo ambalo wakati wote ntajua lakini nilijiskia ilikuwa muda muafaka kuondoka na sijiskii vibaya kwa kufanya hivyo, ni wazi ninakumbukumbu nzuri lakini kwasasa ni mchezaji wa West Bromwich Albion na siwezi kusubiri kucheza".

“Kila mtu aliyehusika kufanya dili likamilike amefanya vizuri na sababu kubwa nipo hapa ni kwasababu ya kocha mkuu, amenivutia kutokea dakika ya kwanza, wakati mtu anapokuonyesha namna anavyokuhitaji ni hisia nzuri”.

Naye winga wa Manchester United Wilifred Zaha ambaye alisajiliwa kutoka Crystal Palace mwaka 2013 kwa ada ya pauni milioni 15 kabla ya kurejeshwa kwa mkopo kwenye klabu hiyo baada ya kushindwa kufanya vyema Old Trafford jana usiku amesajiliwa moja kwa moja na Crystal Palace kwa ada ya pauni milioni sita.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!