Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 February 2015
Saturday, February 07, 2015

Athetico Madrid haina utani yawaadhibu majirani zao
Na Florence George

Mabingwa wateteza wa ligi kuu nchini Hispania klabu ya soka ya Athletico Madrid imeendeleza ubabe kwa msimu dhidi ya mahasimu wao wa karibu klabu ya Real Madrid mara baada ya kuifunga magoli 4-0,mechi iliyochezwa siku ya Jumamosi katika dimba la Vicente Calderon.


Katika mchezo huo kocha wa Real Madrid mtaliano  Carlo Ancelloti alilazimka kuwaanzisha Raphael Varane na Nacho katika sehemu ya beki wa kati kutokana na wachezaji wake tegemeo Sergio Ramos na Pepe kuwa majeruhi.


Pia katika mchezo huo timu ya Real Madrid iliwakosa wachezaji wake muhimu Luka Modric ,James Rodriguez ambao ni majeruhi na Marcelo ambae alikuwa na kadi tano za njano,pia nyota wa timu hiyo Cristiano Ronaldo alirejea uwanjani baada ya kumaliza adhabu yake ya kufungiwa  michezo miwili. 


Athletico walianza kupata goli la kwanza katika dakika ya 14 baada ya Tiago kupiga shuti kali lililomshinda mlinga mlango wa Real Madrid Iker Casillas kabla ya Saul Niguez aliyeingioa kuchukua nafasi ya Coke kufunga goli la pili dakika ya 18,hivyo hadi mapumziko Athletico ilikuwa inaongoza kwa magoli 2-0.


Real Madrid ambao walikuwa hawaonekani kama walikuwa na  mipango ya kusawazisha walijikuta wakifungwa magoli mawili katika kipindi cha pili ,magoli ya Antoine Griezmann na  Mario Mandzukic,hivyo hadi filimbi ya mwisho inapulizwa vijana wa Diego Simeone wanatoka uwanjani wakiwa vifua mbele.Mechi hiyo ilikuwa ya sita kwa timu hizo kukuktana msimu huu ambapo Athletico Madrid imeshinda michezo minne na kutoka sare michezo miwili ambapo mara ya mwisho Real Madrid kuifunga Athletico ilikuwa katika fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya msimu uliopita huko Lisbon nchini Ureno.


Kwa matokeo hayo Real Madrid bado inaongoza ligi ikiwa na pointi 54 katika michezo 22,huku Fc Barcelona ikiwa nafasi ya pili ikiwa na pointi 50 na inatarajiwa kushuka dimbani leo hii kumenyana na Athletic Bilbao na Athletico Madrid ipo katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 50 katika michezo 22 iliyocheza.0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!