Searching...
Image and video hosting by TinyPic
14 December 2014
Sunday, December 14, 2014

Paul Ince azichambua Manchester United na Liverpool.


Na Chikoti Cico

Kuelekea mchezo unaowakutanisha vigogo na wapinzani wa jadi kwenye ligi kuu ya nchini Uingereza kati ya Manchester United dhidi ya Liverpool mchezaji wa zamani aliyewahi kuzichezea timu zote hizo mbili kwa nyakati tofauti Paul Ince azichambua timu hizo na kuonyesha mapungufu waliyonayo.

Paul Ince ambaye alikuwa nahodha wa United huku akiichezea timu hiyo toka 1989-1995 na kushinda vikombe sita chini ya kocha Alex Ferguson akiiongelea timu hiyo chini ya kocha Louis van Gaal alisema “wameshinda michezo yao mitano lakini niliwaangalia dhidi ya Southampton walikuwa wabovu, sikuweza kujua walikuwa wanajaribu kufanya nini”.

“Nafikiri Louis van Gaal anajaribu kufanya kile alichokifanya na Uholanzi lakini hajapata wachezaji wa kufanya hivyo, akiwa na Uholanzi alikuwa na Nigel de Jong kukaa mbele ya eneo la ulinzi ili aweze kucheza 3-5-2 lakini nimewaona United mara mchache msimu huu na sifikiri wana nguvu kwenye eneo la kiungo”

Huku akizisifia timu za Chelsea na Manchester City alisema “Manchester City na Chelsea ni timu nzuri kwasababu wana nguvu sehemu zote uwanjani” Aliendelea kusema “ United wanaposesi mpira uwanjani lakini hawaonekani kama wanaenda popote, kupiga pasi 600 hakukufanyi uwe timu bora siku hizi”

Pia Ince aliichambua Liverpool timu aliyoichezea kwa misimu miwili mwishoni mwa miaka ya 90, Ince aliyefahamika kwa jina la utani la “Gov’nor” alisema “ Ukiachana na Luis Suarez, sielewi kwanini Daniel Agger aliondoka kwenye majira ya joto, nilifikiri alikuwa bora na beki wa katikati wanaotumia mguu wa kushoto hawana bei. Badala ya kutumia pauni milioni 20 kwaajili ya Dejan Lovren wangeokoa hela”

“Ningetumia pesa yoyote kwaajili ya mshambuliaji mkubwa kama Edinson Cavani ama Radamel Falcao kuonyesha kumbadili Suarez na magoli 35 aliyofunga, badala yake wakajaribu kununua wachezaji wapya watano ama sita kugawana magoli lakini haijafanya kazi”

Aliendelea kuongelea umuhimu wa kuwa na washambuliaji bora kwa upande wa Liverpool na kusema “unahitaji washambuliaji wa juu, City wana Sergio Aguero, Chelsea wana Costa hata mkiani mwa msimamo wa ligi QPR wana Charlies Austin na Burnley wana Danny Ings.

Timu kubwa zinahitaji mshambuliaji zaidi ya mmoja. City wakimkosa Aguero wanamleta Edin Dzeko, Liverpool walimpoteza Daniel Sturrridge na hakuna anayefunga”

Mwisho akiongelea mtanange wa leo kati ya Manchester United dhidi ya Liverpool na jinsi makocha wa timu zote mbili watakavyocheza kiungo huyo wa zamani alisema “Nafikiri Van Gaal anaweza kuchezesha mabeki wane na kushambulia dhidi ya Liverpool lakini Brendan Rodgers atapendelea kuishambulia beki ya United”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!