Searching...
Image and video hosting by TinyPic
14 December 2014
Sunday, December 14, 2014

Ni lazima Yanga watatue hili tatizo sugu!


Na Samuel Samuel

0652464525

Moja ya sababu kubwa ya uongozi wa Yanga mwanzoni mwa miaka ya 90 kumleta Raul Shungu ni kurekebisha kikosi ambacho taratibu kilianza kuota mapembe na kujiona ni wafalme hadi kwa viongozi. 

Baada ya ushindi mnono kule Kampala mwaka 1993 Lunyamila, Ngadou Ramadhani, Kizota na wakali wengine kung'ara vilivyo basi kilianza kipindi ambacho timu ilianza kuyumba na hasa uteja kwa Simba SC. 

Shungu anakumbukwa kuunda Yanga Yoso ya kina Anwar Awadhi, Ibrahim, Kalokola na wakali wengine ambao waliweza kuwika na kuweka heshima kubwa Jangwani. 

Mechi ya kukumbukwa ni ndani ya uwanja wa CCM KIRUMBA mkoani Mwanza Simba SC akilala 3-1 huku Akida Makunda aliyesajiliwa toka Simba akionesha thamani ya usajili wake na imani mbele ya maboss wake. 

Achana na Shungu njoo mwanzoni mwa miaka ya 2000 ambapo kwa mara nyingine Yanga inatafuta kocha wa kuokoa jahazi ambalo tayari lilianza kuzama baada ya Simba kuonesha ubabe kwenye ligi ya nyumbani na kimataifa. 

Rudisha kumbukumbu zako nyuma halafu itazame Simba SC mwaka 2003 . Simba iliyomng'oa Zamalekh miamba ya soka Afrika mwaka huo. 

 Baadae mwaka 2004 kombe la Tusker ndani ya uwanja wa zamani wa taifa Yanga inafumuliwa 4-1 na Simba golini akisimama Peter Manyika na beki kisiki Abuu Mtiro akionesha udhaifu mkubwa. 

Viongozi walikaa na kutathimini nani aje aokoe jahazi? Jack Chamangwana kocha toka Malawi huyu alikuja kuokoa jahazi na kuipa Yanga vikombe vya ligi mara mbili mfululizo. 

Sasa kama Brandts mwaka jana alionekana hafai na kulalamikiwa timu haina nidhamu, na haichezi soka la kuvutia kupelekea kufungwa hovyo hasa kupoteza mechi ya mtani jembe mwaka jana 3-1. 

Mbadala wa Brandts Yaanga ilimleta kocha aghari na mwenye mbinu nyingi za ushindi Hans Pluijm. Alifanikiwa sana na klabu hiyo kwa kuipa uwezo wa kufunga magoli mengi , kucheza kitimu na Yanga kuanza kuogopeka Tanzania tatizo lake haikufunga Azam FC wala Simba SC na timu ikaishia mshindi wa pili. 

Lakini hakuna aliyempigia kelele zaidi ya kumwandalia sherehe kubwa ya kumuaga na kumfanya mwanachama wa Yanga. Maximo akaonekana ni mbadala sahihi wa kupokea kijiti cha Hans, wana Yaanga wakiwa na ndoto ya kurudisha kombe lao, kuifunga Azam FC na kuondoa uteja kwa Simba. Je yatatimia ? na kiufundi Maximo ni chaguo sahihi? 

Maximo ni mmoja wa makocha wanaoifundisha Yanga kwa sasa akiwa hana historia yoyote ile nyuma kuipa ushindi wa ligi kuu timu yoyote ile si hapa Tanzania wala nchini kwao Brazil. Ngao ya hisani alilopata na Yanga ndio kikombe cha kwanza katika maisha yake ya soka na timu ya ligi kuu. 

Viongozi wa Yanga na mashabiki wa klabu hiyo ni lazima watambue jambo moja, kama YANGA inahitaji maendeleo kisoka ni lazima wandoe Maximo maana wasitarajie muujiza juu yake. Kwanza kabisa ni kocha ambaye ameonesha udhaifu mkubwa kutengeza muunganiko wa kiuchezaji baina ya wachezaji ndani ya uwanja( playing partnership). 

Unampanga Andrey Coutinho acheze na nani? Una muanzisha Msuva kulia ili katikati apokee nani krosi zake? Niyonzima anacheza namba nane chini kulia kama kiungo mshambuliaji ili atengeneze patterns zipi? 

Pili, kama kocha anashindwa kufanya usajili kulingana na mahitajio ya timu. Alimleta nchini Jaja ambaye ameonesha uwezo mdogo kuendana na kasi ya ligi na mwisho wa siku akajiondokea zake. Coutinho amekuja kufanya nini? hana nguvu, kasi wala uwezo wa kuipenya ngome ya wapinzani zaidi asubiri rebound clearance. 

Kingine ni kukosa saikolojia ya kuijenga timu kiushindi. Kuna kipindi Niyonzima alikaririwa na vyombo vya habari akiulalamikia mfumo wa mwalimu unamnyima fursa ya kuonesha uwezo wake ili aisadie timu. 

Kama Maximo angelikuwa vizuri kisaikolojia basi angeweza kumshawishi mchezaji huyo kuenenda na mfumo wake na mwisho wa siku kupata mafanikio ( flexibility) La mwisho ni kushindwa kabisa kusoma mazingira ya soka la kitanzania katika nyanja mbali mbali hasa miiko yake . 

Huwezi kujiandaa mechi na Simba SC huku ukifanya mazoezi ya wazi. Pili kuamini unajua kila kitu wakati upo ugenini. Samuel

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!