Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 December 2014
Tuesday, December 16, 2014

Kipa wa Chelsea atwaa tuzo nyumbani


Na Chikoti Cico

Kipa namba moja wa timu ya Chelsea yenye maskani yake jijini London Thibaut Courtois atwaa tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka nchini kwao Ubelgiji hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa mwanasoka kushinda tuzo hiyo iliyoanza kutolewa nchini humo toka mwaka 1967.

Courtois aliisaidia timu ya Atletico Madrid kunyakua kombe la ligi kuu nchini Hispania maarufu kama la liga na pia kufika fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya huku akifikisha timu ya taifa ya Ubelgiji kwenye michuano ya kombe la Dunia iliyofanyika nchini Brazili mapema mwezi wa saba huku ikiwa ni muda mrefu toka mwaka 2002 ambapo ilikuwa mara ya mwisho kwa timu hiyo ya taifa kufika kwenye michuano hiyo.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 22 amerejea kuichezea Chelsea kwa msimu huu akitokea Atletico Madrid ambapo alikuwa kwa mkopo na mpaka sasa amiisaidia timu hiyo kushika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza.

Kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo hiyo ya mwanamichezo bora wa mwaka Courtois alipata kura nyingi zaidi huku akimpita mchezaje mwenzake wa Chelsea Eden Hazard aliyekuwa wa tano kwenye listi ya kura zilizopigwa.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!