Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 December 2014
Saturday, December 13, 2014

Frank Lampard amfikia Henry


Na Chikoti Cico

Kiungo wa timu ya Manchester City Frank Lampard afikia rekodi ya magoli ya mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Thiery Henry baada ya kuifungia Manchester City goli la ushindi dhidi ya Leicester City kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza.

Huku likiwa ni goli lake la sita toka aliposajiliwa kwa mkopo toka New York City FC hivyo Lampard alifikisha magoli 175 sawa sawa na Henry na wote wawili kushika nafasi ya nne katika listi ya wafungaji bora wa muda wote kwenye ligi kuu nchini Uingereza.

Akiongelea kufikia rekodi hiyo ya Henry baada ya mchezo dhidi ya Leicester City, Lampard alisema “ ninafuraha katika hilo, nilifikiri ingekuwa nje ya uwezo wangu kufikia (rekodi). Nina heshima kwa Henry ni mmoja wa wachezaji wakubwa kwenye historia ya ligi ya Uingereza na kuwa naye pale juu ni vizuri sana”

Lampard ambaye ana miaka 36 amefikisha magoli hayo 175 akizichezea timu za West Ham, Chelsea na Manchester City kwenye ligi ya Uingereza huku akiichezea timu ya Chelsea kwa miaka 13 kabla ya kusajiliwa nchini Marekani na timu ya New York City FC.

Huku Lampard na Henry wakishika nafsi ya nne kwenye listi ya wafungaji bora wa muda wote katika ligi ya Uingereza, Alan Shearer mwenye magoli 260 anashika nafasi ya kwanza, Andrew Cole anashika nfasi ya pili akiwa na 187 na nahodha wa Manchester United Wayne Rooney anashika nafasi ya tatu akiwa na magoli 178.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!