Searching...
Image and video hosting by TinyPic
14 December 2014
Sunday, December 14, 2014

Arsenal yaigaragaza Newcastle


Na Chikoti Cico

Katika mfululizo wa matokeo ya mechi za ligi kuu nchini Uingereza zilizopigwa siku ya Jumamosi timu ya Arsenal iliibuka kidedea kwa ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Newcastle mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Emirates.

Arsenal walianza mchezo huo kwa kasi na iliwachukua dakika 15 tu toka kuanza kwa mchezo kupata goli la kwanza lililofungwa na Olivier Giroud akiunganisha kwa kichwa krosi iliyochongwa na Alexis Sanchez baada ya goli hilo mchezo uliendelea kwa kasi huku Arsenal wakiendelea kulisakama lango la Newcastle lakini mpaka mapumziko Arsenal walikuwa mbele kwa goli hilo moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na kila timu ikijaribu kutafuta goli huku Newcastle kupitia Papiss Cisse wakifanya mashambulizi ya hapa na pale kujaribu kutafuta goli la kusawazisha bila mafanikio lakini walikuwa ni Arsenal tena walioandika goli la pili kupitia kwa Santi Carzola akipokea pasi kutoka kwa Sanchez tena.

Baada ya goli hilo la pili Arsenal waliendelea kutawala mchezo huo na kwenye dakika ya 58 krosi iliyochongwa na Hector Bellerin ilimkuta Giroud tena na kuiandikia Arsenal goli la tatu, goli liliwanyong’onyesha zaidi vijana wa kocha wa Newcastle Alan Pardew.

Pamoja na kupata goli la kufutia machozi kwenye dakika ya 63 kupitia kwa Ayoze Perez lakini bado Newcastle hawakuweza kuwamudu tena washika bunduki hao wa London na goli la Carzola kwenye dakika ya 88 akifunga kwa njia ya penati liliihakikishia timu ya Arsenal alama tatu muhimu nyumbani Emirates.

Mwamuzi wa mchezo huo Lee Mason aliwaonyesha kadi za njano Bellerin na Oxlade-Chamberlin kwa upande wa Arsenal huku pia akiwaonyesha Tiote na Janmaat kwa upande wa Newcastle na mpaka mwamuzi huyo anapuliza kipenga kumaliza mchezo huo Arsenal waliondoka kifua mbele uwanjani.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!