Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 March 2014
Friday, March 21, 2014

YANGA KUITEKA TABORA KESHO



Kikosi cha Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans kesho kitashuka katika dimba la Ally Hassan Mwinyi mjini wa Tabora kucheza na wenyeji timu ya Maafande wa Jeshi la Ulinzi Nchini Rhino Rangers mchezo utakaopigwa majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Tayari Young Africans imeshawasili mjini Tabora tangu jana usiku na kufikia katika Hoteli ya Orion (Tabora Hoteli) huku leo asubuhi majira ya saa 4 wachezaji wakifanya mazoezi katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi tayari kabisa kwa mchezo huo.

Young Africans itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare mbili mfululizo dhidi ya Mtibwa Sugar na Azam FC matokeo ambayo yameifanya iendelee kubakia katika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya vinara wenye ponti 44 timu ya Azam FC.

Makocha wa Young Africans Hans Ver Pluijm na Charles Mkwasa wamesema vijana wao wapo katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo wa kesho, kuna mapungufu yalijitokeza katika michezo iliyopita wameshayafanyia kazi na wanaamini kesho wataibuka na ushindi mzuri.

Bado tuna nafasi kubwa tu ya kutetea Ubingwa wetu kwa msimu wa pili mfululizo, na kwa maana hiyo tunahitaji kupata ushindi katika mchezo dhidi ya Rhino Rangers ambao pia wapo katika mstari wa kushuka daraja na wao wakihitaji kupata pointi ili kuweza kujinasua kwenye sehemu ya hatari.
Jumla ya wachezaji 19 wapo mjini Tabora pamoja na benchi la Ufundi na viongozi wakifamalizia maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo huo.

Wachezaji waliopo na timu mjini Tabora ni:

Juma Kaseja na Ally Mustapha "Barthez"
Juma Abdul, Ibrahim Job, Oscar Joshua, David Luhende, Nadir Haroub "Cannavaro", Kelvin Yondani,
Viungo: Frank Domayo, Athumani Idd "Chuji", Hassan Dilunga, Nizar Khalfani na Haruna Niyonzima 
Washambuliaji: Saimon Msuva, Mrisho Ngasa, Hussein Javu, Hamisi Kizza, Emmanuel Okwi, Jerson Tegete

Wachezaji Deo Munish "Dida" na mshambuliaji Dider Kavumbagu hawakuweza kusafiri na timu kutokana na kuwa majeruhi ambapo wamebakia jijini Dar es salaam wakiendelea kupata matibabu huku mlinzi Mbuyu Twite akitarajiwa kuungana na wenzake pindi watakaporejea jijini Dar es salaam siku ya jumapili.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa website ya YANGA.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!