Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 March 2014
Friday, March 21, 2014

KOCHA WA GHANA AMETUWA LIVERPOOL



Kocha wa timu ya taifa ya Ghana, Kwesi Appiah yuko ziarani nchini Uingereza kupata uzoefu kutoka kwa klabu ya soka ya Liverpool.
Appiah pamoja na kocha wa golkipa Nassam Yakubu, watajionea Liverpool inavyofanya maandalizi kabla ya michuano yoyote.
Zaidi ya hayo kocha huyo wa Black stars, atakutana na maafisa wa shirikisho la mameneja katika uwanja wa St. George, kituo cha mazoezi ya timu ya taifa ya soka ya England.
Ziara hii inalenga kusaidia maandalizi ya timu ya taifa ya Ghana kabla ya kushiriki michuano ya kombe la dunia.

Ujumbe huo unajumuisha naibu wa Appiah, Maxwell Konadu, Yakubu, daktari wa kikosi hicho, Adam Baba na mdadisi Michael Okyere.
Walitarajiwa kuondoka Accra jana kwa ziara hiyo itakayodumu siku kumi.

"hii ni fursa nzuri sana kwetu kuweza kutembelea Liverpool,moja ya vilabu mahiri vya soka duniani kujionea wanavyojiandaa kabla ya michuano,'' alisema Rais wa shirikisho la soka nchini Ghana Kwesi Nyantakyi.
"bila shaka fursa hii itakua muhimu sana kwa kikosi cha Black Stars na itawasaidia kuleta nyumbani ushindi.''

Sio mara ya kwanza kwa Appiah kuzuru England ili kuboresha uzoefu wake na wa wachezaji, amewahi kutembelea Manchester zaidi ya mara moja.
Ghana iko katika kundi G katika michuano ya kombe la dunia pamoja na Brazil na Ujeumani , Ureno na Marekani.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!