NIONAVYO MIMI KWA FRANCIS CHEKA NA SOKA LA BONGO.
Na Oscar Oscar Jr
0789-784858
Bondia wetu CHEKA hivi karibuni alitangaza nia yake ya kujiendeleza
kielimu.Ataanza na pre-form na baadae mpaka chuo kikuu,binafsi namtakia
kila la kheri.
Anachofanya CHEKA ndicho tunachoshindwa kwenye
soka,hatuna CREDITS na hatutaki ku-resit wala kurudia darasa kabisa.kuna
uwezekano CHEKA akafika form four kabla ya sisi kucheza AFCON!
Ni rahisi kwa Francis Cheka kwenda chuo kikuu kuliko TAIFA STARS
kucheza kombe la Dunia,Ni rahisi kwa Francis Cheka kupata PHD kuliko
STARS kutwaa kombe la AFCON,Ni rahisi kwa CHEKA kuwa professor kuliko
STARS kutwaa kombe la Dunia!!
Binadamu anahitaji zaidi akili,Pesa na Elimu ni ziada tu.
I'm sorry!
16 November 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment